Tuesday, May 28, 2013

MSANII ALIYEKUA NA MAREHEMU NGWEA YUKO MAHUTUTI HOSPITALI, NI M TO THE P MADKATARI WAPANGA KUICHOMOA MIPIRA BAADA YA MASAA SABA


Kutoka kushoto ni Marehem ALBERT MANGWEA NA M 2 THE P
Msanii aliyekua na Mangwea kabla hajalala na kuaga dunia, M 2 the P tumefahamishwa kuwa yuko mahututi hospitali na anapumulia mashine katika wodi ya wagonjwa mahututi, inasemekana kwamba madaktari wamepanga kwamba yakipita masaa saba akiwa bado hajazinduka basi itabidi waichomoe mipira inayomsaidia kupumua, hiyo ikimaanisha kuwa msanii huyo atakua ameaga dunia, inasemekana M 2 The P kabla ya kuwa katika hali hiyo ya kupoteza fahamu, jana usiku walirudi mahala ambako walikua wanaishi yeye marehemu Ngwair, wakalala na wenzao ila asubuhi kulipokucha wawili hao walishindwa kuinuka ndipo washkaji wakajaribu kumzindua Ngwair bila mafanikio na M 2 the P ndo alikua afadhali kidogo lakini mahututi wakapelekwa hospitali Ngwair alikua kishafariki dunia na M2 the p hali yake ilikua mahututi, Hiyo ni kwa mujibu wa mdau wa muziki anayefahamika kwa jina KINJE mtoto wa Kingunge Ngombale Mwiru aliyeongea jioni hii na Mtangazaji wa Clouds fm Hamis Mandi a.k.a B 12  mungu ailaze roho ya marehem Albert Mangwea Peponi amina, na mungu amponye M 2 The P

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.