|
GELLY WA RHYMES |
Msanii wa bongo flava Gelly wa Rhymez usiku wa kuamkia jumapili iliyopita inasemekana kwamba eti alishambuliwa na mtu aliyevamia nyumbani kwake na kumkuta na dem, habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema kwamba eti siku ya tukio mishale ya saa kumi ucku msanii huyo alirudi pale anapoishi maeneo ya Sinza jijini Dar es salaam huku akiwa ameambatana na mlimbwende matata sanaaaa, sasa haikupita hata nusu saa mara ikaskika hodi, jamaa akazama ndani ya Gelly bila kukaribishwa akaanza kutifua kwa kuanza kumfokea mwanamke huyo huku Gelly akiwa kwenye taswira ya upole akaanza kumwelewesha yule jamaa kwa kumwambia walikua hawafanyi kitu chochote na yeye na dem huyo ni marafiki wa kawaida, mchizi huyo aliyekua amejazia utadhani Kalapina akaanza kumshushia cherehani/ ngumi na mateke Gelly wa Rhymes na kumpasua sehemu za juu ya jicho, mwanamke akamwambia bwana wake wamsaidie msanii huyo kwa kumpeleka hospitali, jamaa huyo alichomoa katu katu, kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari mchizi huyo alikua anadai mwanadada huyo ni mke wake na lijama linaitwa Geofrey.