Tuesday, May 14, 2013

VIDEO : KUMBE SLIM WA BONGO MOVIE ANAISHI NA VYUMA MWILINI


Actor wa bongo movie anayefahamika kwa jina la SLIM kupitia kipindi cha Take One ya Clouds TV ametiririka kuwa moja kati ya vitu ambavyo hatakuja kuvisahau maishani mwake ni baada ya kupata ajali ya bodaboda/ pikipiki iliyosababisha mfupa wa mguu wake ukatike kabisa, hivyo madaktari wakamwekea chuma kikubwa mguuni, Slim amesema hawezi kusahau kwasababu ilisababisha akae kitandani kujiuguza kwa mwaka mzima bila kufanya kazi, akaongeza kuwa anampango wa kukitoa chuma hicho ila anasubiri apige mkwanja kwanza kwasababu akikurupuka kufanya hivyo sasa hivi itamlazima akae miezi miwili bila kufanya kazi.
zaidi mskie anavyofunguka katika video hiyo.
Story kwa hisani ya CLOUDSTV

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.