Lulu Katika Chumba cha Mahakama |
Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabiri muigizaji wa kike,
Elizabeth Michael maarufu kama Lulu imesikilizwa leo (February 17)
katika mahakama kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Lulu alikiri mbele ya Jaji Rose Temba kuwa alikuwa na uhusiano wa mapenzi na marehemu Steven Kanumba na kwamba walikuwa na ugomvi, lakini alikana mashitaka ya kumuua bila kukusudia.
MWANASHERIA WA LULU NDUGU KIBATARA AKITETA JAMBO NA LULU |
Akisoma hati ya mashitaka, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Monica
Mbogo, alidai kuwa Aprili 7, mwaka 2012, Sinza Vatikani, Mkoa wa Dar es
salaam, mshitakiwa alimuua bila kukusudia Stevin Kanumba.
Wakili Kombo, alidai kuwa pamoja na mambo mengine, marehemu Kanumba
baada ya kufa, mwili wake ilipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo
majibu yanaonyesha kwamba kifo chake kimesababishwa na uvimbe ndani ya
ubongo.
Upande wa serikali una mashahidi watano pamoja na vielelezo wakati upande wa utetezi pia unatarajia kuwa na mashahidi watano na vielelezo.
KULIA DR CHENI WA PILI KULIA NI LULU NA MAMA YAKE LULU WA TATU KULIAWAKIWA KATIKA CHUMBA CHA MAHAKAMA KUU LEO |