Producer Mswaki |
kwa mujibu wa mswaki anadai kuwa miaka ya nyuma wakati Ngwea akiwa Hai aliwahi kumkataza asitumie style hiyo, akisimulia mkasa huo ulivyokua Producer Mswaki anasema yeye amekulia Mjini Dodoma na alikua anapenda sana nyimbo za Ngwea akajikuta anaandika Lyrics za nyimbo za Ngwea na kuziimba kwa muda mrefu mpaka akajikuta hata mistari yake anai andika kwa style ya Ngwea,
Na kwenye baadhi ya Radio za Dodoma akawa anaitwa ili akafanye Jingle kwa sauti ya Albert Mangwea, mpaka siku moja akapigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Ngwea na kumwambia asifanye michezo hiyo, Mswaki anasema aliacha kuiga Style ya Ngwea, lakini kutokana na mapenzi yake kwa msanii huyo alipokufa ndio akaja na wazo la kuufanya muziki wa Ngwea uwe Hai kumuenzi kwa kutumia style yake, kwani bila hivyo baada ya miaka flani Muziki wa Ngwea na Habari zake zinaweza kusahaulika.
Ngwea |
Mswaki akamalizia kwa kusema kuwa ana mpango wa Kwenda kwa kina Albert Mangwea ili akapate baraka za familia hiyo, na iwapo watakubali basi Mkwanja utakaopatikana kwenye Mauzo ya Album anayoifanya kiasi cha pesa kitaenda kwa mama mzazi wa Albert Mangwea R.I.P