Wednesday, March 12, 2014

RUKKII ANA DAWA YA WEZI WA PAGE ZA FACEBOOK





Asilimia 99 ya matukio ya celebrities kuibiwa account zao za facebook mwisho wa siku huwa wanashindwa kurudisha account zao kwenye himaya, lakini msanii aliyeimba wimbo wa “MIMI NA WEWE” mwanadada Rukkii hivi karibuni alichezeshewa mchezo kama huo na hackers na mwisho wa siku yeye na management yake walifanikiwa kuirudisha account hiyo ambayo tayari ilishaanza kutumika vibaya kwa kuwatapeli watu eti amewahi kupata mkopo kwenye taasisi inayomilikiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, na watu wengine wakawa wanashawishiwa wakope lakini hutakiwa kutoa kiasi flani cha pesa ili wapate mkopo, wakati Zitto Kabwe hana taasisi kama hiyo, Rukkii anasema alihangaika kwa siku kadhaa bila mafanikio ndipo alipoamua ku report tukio hilo kwa management yake ,wakafanikiwa kuirudisha account hiyo…….

Awali Hackers walifanikiwa ku hack account hiyo baada ya kumtumia Link Rukkii na kumwambia eti picha zake za usagaji zimebambwa na ili azione abonyeze link hiyo, na yeye alibonyeza kweli hatimaye siku nyingine alipotaka kusign in akashindwa

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.