Tuesday, March 25, 2014

YOU HEARD: TAPELI WA GEEZ MABOVU ATEKWA MBELE YA MADEE

Baada ya jaribio lake la utapeli kugonga mwamba Kwa Madee, Tapeli Musa aelezea sababu za kutumia jina la Geez Mabovu kwenye shughuli zake, Awali inadaiwa Kijana Musa (20) alimpigia simu Msanii wa Bongo Flava Madee na kujitambulisha kama yeye ni ndugu wa damu na Rapper Geez Mabovu, Musa akaendelea kutiririka kuwa eti Geez anaumwa na figo yake moja ishafeli kwa hiyo anatakiwa kubadilishiwa figo kwenye hospitali nchini Kenya, Musa bila haya akasema kuna mtu wa kujitolea figo amepatikana mkoani Iringa kwa hiyo gharama zote hizo ni milioni 7 na familia imejipiga piga wamepata milioni 3 kwa hiyo wanaomba wasanii na wadau wamchangie milioni 4 zilizobaki, Madee baada ya machale kumcheza akamvuta yule tapeli mpaka maskani kwa Manzese, Tapeli Musa nae bila kujua akaibuka pande zile kichwa kichwa, kufika kule ikapigwa simu kwa Geez Mabovu ambaye muda huo alikua Iringa, Geez alifunguka kuwa ni kweli alikua anaumwa malaria na sio figo na alishapona siku nyingi, Raia wa Manzese alimvua nguo zote Tapeli Musa na kumpiga sanaaa, Nilifanikiwa kupiga story na Musa na akaniambia kuwa chanzo cha yeye kuamua kutapeli kwa style hiyo anasema amekua akiimba Bongo Flava kwa muda mrefu lakini hajawahi kufanikiwa kupata pesa ya kurekodi, mara ya mwisho akaenda Studio za Sharobaro Magomeni mapipa akakutana na Producer Bob Junior na kuambiwa gharama za kurekodi pale ni shilingi laki 5, eti ndio maana akaamua kuusaka mkwanja huo kwa udi na Uvumba, Raia waliendelea kumfanyizia mpaka Madee meneja wa TMK Saidi Fela na Babu Tale wakaingilia kati kwa kumnusuru Tapeli Musa saa moja baadae wakajisahau wakatokea watu wengine wasiofahamika wakamteka Tapeli Musa na kutokomea kusikojulikana.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.