Sekta ya bongo movie
imepoteza jembe lingine rachel haule, aliyefariki leo asubuhi kutokana
complication zilizotokea jana usiku baada ya kujifungua kwa operation , mtoto
akafariki na rachel akalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, ilipofika asubuhi ya leo Rachel Haule akaaga dunia.
Amewahi kucheza filamu nyingi
kama: Siku za majaribu, mtihani, na movie za odama chini ya Kampuni J film for life, na filamu ya hivi
karibuni kucheza ilikua Vanesa in Dillema.
Leo
asubuhi wasanii wa bongo walikutana pale Leaders club pamoja na maelezo
kutoka kwa ndugu wa marehemu ikaamuliwa kuwa mwili wa Recho Haule
utasafirishwa kwa ajili ya maziko pamoja na mwili wa mtoto wake mchanga
aliyefariki kuelekea Songea ambako kuna bibi yake pamoja na mtoto wake
mkubwa, wazazi wa Recho Haule walifariki siku nyingi.