Wednesday, July 23, 2014

HAMIS MANDI ( B TWELVE) ASHEREHEKEA BIRTHDAY YAKE KWA KULA FUTARI NA WATOTO YATIMA

 Mtangazaji wa Kipindi cha XXL ya Clouds fm Hamis Mandi a.k.a B 12 / B Dozen jana alikua anasherehekea kumbukumbu yake ya siku ya Kuzaliwa (Birthday) na aliamua kuitumia siku hiyo kwa kwenda kufuturu na Watoto Yatima wa Kituo cha Chakuwama kilichopo Sinza Mori, B 12 aliambatana na baadhi ya marafiki zake kadhaa wakiwemo wasanii wa Bongo Flava Shilole, Bob Junior, Nuh Mziwanda, Hamza Balla kutoka T.H.T, Meneja wa Msanii Samir anaitwa Sadick pia walikuwepo waandishi wa habari na Wapiga Picha kutoka Clouds Media Group alikuwepo Bestizo, Soudy Brown, kutoka Global Publishers alikuwepo Zungu na Musa Mateja, na Kutoka Mtandao wa Millard Ayo alikuwepo Edwin Elinema.
Baada ya kufika kwenye kituo hiki chenye watoto 80 ilikua ni mida ya saa kumi na mbili jioni B 12 alianza kupiga stori na watoto hao ilipofika time ya kufuturu akaanza kugawa chakula  alichokua amekuja nacho kikiwa tayari kimepikwa, watoto walifurahi sanaaa na kujipanga mstari kwa utaratibu, baada ya kupiga msosi akaikata keki na kuwalisha watoto, wasimamizi wa kituo pamoja wasanii waliofika katika tukio hili.
Hamis Mandi / B12 akakabidhi msaada ya Chakula cha Eid El Fitr Mchele kilo 200, Sukari na Mafuta.
Ratiba ikaisha mida ya saa mbili usiku.











Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.