Wednesday, July 23, 2014

BABA LEVO ADAIWA KUMPIGA SHEMEJI YAKE MSIBANI

Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MSANII wa Bongo Fleva Baba Levo anadaiwa kumpa kichapo cha haja shemeji yake Pili Kimenya ambaye alikuwa ni mchumba wa marehemu mdogo wake Patrick Revocatus akidai kupewa cheni ya silver ambayo ilikuwa ya mdogo wake aliyoondoka nayo shemeji yake.
vurugu hizo zilitokea nyumbani kwao na baba Levo katika nyumba ya familia iliyopo mtaa wa Kisangani Mwanga mjini Kigoma ambapo msiba wa marehemu ulikuwa umewekwa.

Akisimulia msala huo Pili Kimenya ambaye alikuwa shemeji yake na Baba Levo alisema kuwa anashangazwa na kitendo cha madai ya Baba Levo kumtuhumu kuondoka na chrni hiyo ya Silver inayodaiwa kuwa na gramu 25 mali ya marehehu.
Kufuatia kichapo hicho Pili alifungua jalada katika kituo kidogo cha polisi Kisangani mjini Kigoma na kupewa RB namba KGC/RB/2819/014 ambalo linahusu shambulio la kudhuru mwili.
Baada ya hapo alipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa Kigoma Maweni na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Gazeti La Makorokocho lilipomtafuta Baba Levo alikanusha taarifa hizi na kudai kuwa siku ya tukio Pili na Mama yake walivamia kwenye msiba wa kaka yake na kufanya fujo ndipo yeye akaamua kuwafukuza na kwenda kutoa taarifa polisi kisha Pili Na Mama yake wakakamatwa ikabidi wazee wa mtaani waende kumwomba Baba Levo awasamehe wanawake hao..
Baba Levo akawasamehe na kuendelea na msiba.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.