Taarifa zilizohit kwenye mtandao wa Makorokocho zinadai kuwa eti
Wimbo wa Kundi la Weusi unaitwa "Gere" eti Mdundo wake ni Copy ya wimbo
wa Msanii wa HipHop kutoka Cleveland Marekani anayeitwa Machine Gun
Kelly na wimbo wake unaitwa Peso amewashirikisha Ma rapa Meek Mill na
Pusha T uliotoka mwanzoni mwa mwaka 2013, akizungumzia Ishu Hii Rapper
Joh Makini amekanusha na kupiga pasi kwa Mtaarishaji wa wimbo wa Gere Producer Nahreel kwa sababu yeye ndiye aliyehusika kwenye Upishi wa ngoma nzima, kwani wao waliikuta beat imeshatengenezwa.
Producer huyo alipovutiwa Wire na Gossip Cop Tz aliruka
futi mia na kudai kuwa tuhuma hizo si za kweli kwasababu kama yeye
angekua anatabia mbaya za ku copy midundo ya watu basi ingejulikana siku
nyingi.
Wimbo wa Gere Umetoka mwishoni mwa Mwaka jana na kufanya vizuri kwenye chart za radio mbalimbali sambamba na video ya ngoma hii pia imefanya vizuri pia.
 |
Machine Gun Kelly |
 |
Producer NahReel wa Switch Records |
SKIZA WALICHOONGEA KUPITIA YOU HEARD YA XXL CLOUDS FM