Friday, August 1, 2014

TOP 5 YA WATOTO MATAJIRI DUNIANI

#1 Robert Nay

 
Mwaka 2011 Robert akiwa na umri wa miaka 14 ali release Game yake ya Kwanza yenye uwezo wa kuingia kwenye simu za mkononi inaitwa Bubble Ball na Game hiyo ni maarufu kwenye mtandao wa itunes ndani ya wiki mbili ikapakuliwa mara milioni 2, na alitengeneza zaidi ya dola laki 2 na 47 elfu kipindi hiko akiwa darasa la 8.

#2 Asya Gonzalez

 
Asya Gonzalez alizindua Mashati yake aina ya "Stinky Feet Gurlz"  akiwa na na umri wa miaka 13, na amekua akipata sehemu ya mauzo ya kila shati linalouzwa pesa yake imekua ikienda  kusaidia kwenye kampeni za kuwaondoa watoto kwenye biashara ya ngono, na mashati hayo yanakadiriwa kuja kumwingizia dola elfu 20 kwa mwezi.

#3 Nick D’Aloisio

Nick D’Aloisio alitengeneza App ya habari akiwa na umri wa miaka 17, lakini akiwa na msaada wa watu wachache. mwanzoni mwa mwaka 2013, Kampuni ya Yahoo ilinunua haki za app hiyo kwa dola milioni 30. kama sehemu ya dili hilo D’Aloisio alipewa kazi na Yahoo kwa miezi 18. 

#4 Anshul Samar

 

 Anshul Samar akiwa na darasa la 8 alianzisha kampuni yake ya Alchemist Empire na kutengeneza Karata (Elemento) zinazofundisha somo la Chemistry, sasa hivi mtoto huyu anasoma lakini karata zake zimetengenezewa App, na kiasi cha pesa anachopata anakigawanya kwa kusaidia wanafunzi wajasiriamali na inakadiriwa utajiri wake ubnafikia dola milioni 4.

#5 Leanna Archer

Leanna Archer alianzisha kampuni ya Leanna’s Inc., akiwa na umri wa miaka 8. Leanna’s Inc inauza bidhaa za nywele zikiwa na mchanganyiko (Formula) ambao umebuniwa na familia yake na kurithishana vizazi na vizazi  na sasa hivi bidhaa hizo zinauzwa kupitia kwa wasambazaji na masaluni ya kike, kwa mwaka Leanna’s Inc inatengeneza faida ya zaidi ya dola laki moja kila mwaka.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.