Thursday, December 18, 2014

POLISI WAZUIA MAZISHI YA AISHA MADINDA, KIFO CHAKE KINA UTATA

Mazishi ya Aisha Madinda ambayo yalitarajiwa kufanyika leo jijini Dar es salaam yameahirishwa mpaka matokeo ya uchunguzi wa kifo chake yakamilike, Wanandugu waliamua hivyo baada ya kuhisi labda kuna mkono wa mtu, nilipozungumza na mtoto wa kwanza wa marehem anayeitwa Feisal anasema yeye ana hisi kuna kitu kimesababishwa na kutokea kwa kifo cha mama yake, kwani siku moja kabla mama yake hajakutwa na mauti aliwasiliana nae na akamwambia kuwa yuko na mwanadada flani jina kapuni ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi, Feisal anasema siku hiyo mama yake alikua mzima na wala hakuonyesha kuwa anaumwa, na siku ya pili Feisal akapigiwa simu kuwa mama yake amepelekwa hospitali ya mwananyamala, 

ikabidi awahi hospitalini hapo na kuwakuta ndugu na jamaa wakiwa wanamhoji Dada nonihino (anayeshikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi) na dada huyo alikua anadai hafahamiani na marehem ila alimkuta eneo flani akiwa ameanguka kwa hiyo yeye kama msamaria mwema akaamua kumsaidia kwa kumnyanyua na kumwahisha hospitali, ndipo Feisal akamuuliza unaitwa nani kwani? alipojibiwa ndipo akakumbuka mama yake alimwambia kuwa yupo na mwanadada anayeitwa jina kama hilo, so iweje huyu dada aseme hakuwa akifahamiana na marehemu? utata ndio ukaanzia hapo, polisi wakamchukua kwenda kumhoji vizuri.... 
sikiliza Sauti ya Feisal akifunguka hapo chini.......

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.