Wema Sepetu anasema wakati yupo katika mahusiano na Diamond Platnumz alikua hana uwezo kufikiria kuhusu maendeleo yake binafsi, na tangu waachane miezi kadhaa iliyopita ndio ameweza kufanya vitu vingi kwa ajili ya maisha yake, vitu hivyo ni pamoja na Concerts za Endless Fame pamoja na Movie aliyoshirikiana na muigizaji wa Ghana Joseph Van Vicker, Wema Sepetu alizungumza hayo baada ya kuulizwa na Gossip Cop "kwanini amekua busy na project zake muda mfupi baada ya kuachana na Diamond, kwanini wakati yupo na Diamond hakua hivi? .....
Wema Akaulizwa tena "Je Unapoona picha za Diamond na Zari The Boss Lady unajisikiaje moyoni?
Wema akajibu "Sioni Wivu na nawatakia maisha mema"
sikiliza Interview hiyo iliyofanyika kwenye utambulisho wa msanii mpya wa Endless Fame Ally Lunya uliofanyika Club 71 Kibo Complex tarehe 28 December 2014, Show iliyosindikizwa na wasanii kibao kama Bob Junior, Godzilah, Izzo Business, Barnaba Boy, Linex na Mirra.