Kampuni ya Mtandao wa simu ya Vodacom Tanzania imezindua promosheni kubwa ya michezo wa bahati nasibu ambapo wateja watajishindia pesa Sh. bilioni 30/- kama zawadi ndani ya kipindi cha siku 100.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema promosheni hii inajulikana kama JayMillions na inawahusisha wateja wote wa Vodacom.
Katika promosheni hii Vodacom itatoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/- washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi mia moja wa Sh. 1m/- kila siku, hii itakwenda kwa muda siku mia moja, huku washindi wengine elfu kumi wakijishindia muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/- kila siku.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa amesema ili kushiriki katika promosheni hii, mteja yeyote wa Vodacom anahitaji kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda namba 15544 kila siku ili kujua kama ameshinda au hapana.