Siku ya jana January 13 Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania iliandika historia kubwa na nzuri ambayo ni ya kwanza tangu tuingie 2015.
Vodacom walikutanisha watu wa nguvu pale Double Tree, Masaki Dar es Salaam, usiku wa jana kwa ajili ya shughuli yote ya uzinduzi wa Promosheni ya #JayMilions.
Unaambiwa kwamba huu ni mchezo wa bahati
nasibu ambapo wateja watajishindia pesa Sh. bilioni 30/- kama zawadi
ndani ya kipindi cha siku 100, namna ya kujiunga unaweza kutuma sms
yenye neno ‘JAY’ kwenda namba 15544 ambapo utajua pia kama wewe ni mmoja
ya washindi wa siku hiyo.
Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde akiwa na MC Pilipili.