Baada ya sokosoko kuu la kwanini?? muda wote huu kijana Nassib Abdul – Diamond Platnumz pamoja na list yake ndeeeefu ya mabinti wa bongomovies aliowahi kutembea nao hajawahi kuwa hata na mtoto wa kusingiziwa, HATIMAYE jana kupitia kwenye nyezo za kiteknolojia tumeweza kudokezwa juu ya ujauzito alionao mwanadada ZARI ambao ni fika utakuwa wa kijana huyu anayetamba na wimbo wa “Nitampata wapi” ambao wachunguziwa mambo wanadai ETi ni dedication kwa mpenzi wake maarufu wa zamani.
USHAHIDI WA UJAUZITO HUO
Usiku wa jana, Dimaond aliweka ujumbe unaosema “I can not wait to have you on my hands #Chibu_Junior” akimaanisha “siwezi kusubiri kukuweka kwenye mikono yangu #Chibu_Junior” huku akiambatanisha na picha ya Ultra sound aliyoupiga na Zari (Kama hujui Ultra sound ni nini Tafadhali google) na baadaye Zari naye akapost picha yake akichukuliwa vipimo hivyo bila kuandika kitu chochote na kuwaacha wananchi wakimwagika na comment za kutosha kuhusu picha hizo ambazo fika zinaonesha wawil hao wanaweza kujaliwa mtoto mwaka huu
Je unafikiri hii inaweza kuwa “Project nyingine” au ni kweli wawili hawa wanatarajiwa kuwa wazazi?? Tupe maoni yako