Mwanamitindo wa Tanzania ambaye anaishi na kufanya shughuli zake Marekani, Flaviana Matata ni mmoja ya mastaa ambao wanaendesha Foundation ambazo hutoa misaada mbalimbali ya kijamii.
Taasisi ya mwanamitindo huyo Flaviana Matata Foundation (FMF)
imeanza kutoa misaada kama namna ya kusaidia kuboresha elimu katika
shule, ambapo jana January 13 walitoa msaada wa vitu mbalimbali Shule ya
Msingi Msinune iliyopo Bagamoyo katika ule mpango uliopo kwa taasisi
hiyo kusaidia wanafunzi vitu mbalimbali ikiwemo mavazi, majengo, vyakula
na vifaa vya shule.
Mwaka 2014 Taasisi ya FMF ilisaidia wtoto 3000 kwa
kuwapatia vifaa vya kujifunzia ambapo mkakati wao mwaka huu ni kuendelea
kutatua changamoto mbalimbali za wanafunzi kwa kuwapatia misaada
mbalimbali katika mikoa ya Shinyanga, Lindi na Arusha.
Kwa yeyote ambaye anahitaji kuwasilisha mchango wake kwenye Taasisi hiyo anaweza kuwasiliana nao kupitia;
info@flavianamatatafoundation. org au simu namba +255 784 200 680