Imefahamika kwamba chanzo cha mwanamitindo wa kiitaliano Fanny Naguesha kumpiga chini aliyekuwa mchumba wake mchezaji wa Liverpool - Mario Balotelli ni kutokana na mwanasoka huyo kumkataza Naguesha kuendelea na modelling. Balotelli alimvalisha pete ya uchumba Naguesha wakati wa kombe la dunia mwaka jana nchini Brazil lakini uhusiano wao ukaishia njiani baada ya Balo kuingilia kazi ya mwenzie.