Sunday, January 25, 2015

D BANJ KUSIMAMISHWA KIZIMBANI


Staa wa Muziki wa Pop toka Nigeria, D’Banj anadaiwa kufikishwa mahakamani kabla ya mwezi huu kwisha kufuatia kesi ya deni analodaiwa kutoka kwa kigogo maarufu wa  vituo vya gesi na mafuta vya nchini humo, Henry Ojogho.
Chanzo kilidai kuwa D’Banj alikopa kiasi cha Naira milioni 60 mapema mwaka 2013, lakini alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha jambo lililopelekea kigogo huyo kumfungulia kesi ya madai na kutakiwa kufika mahakamani  Desemba 17 mwaka jana, kabla ya kesi hiyo kuahirishwa na kupangwa mwishoni mwa mwezi huu.

Akijibu tuhuma hizo msemaji wa mwanamuziki huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alikanusha tuhuma hizo na kudai siyo za kweli.
Kama hiyo haitoshi mtandao mmoja ulitupia picha za siri uliozinasa unaonesha wito wa mahakama ukimtaka D’Banj afike mahakamani huku ushahidi mwingine wa picha za msanii huyo akiwa mahakamani ukitajwa kuwepo.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.