Sunday, January 25, 2015

KANYE WEST AFUNGUKA KWA NINI HATABASAMU


Rapa wa kimataifa toka nchini Marekani, Kanye West amefungukia sababu inayomfanya asipende kutabasamu hasa akiweka pozi mbele ya mapaparazi na kudaiwa kuwa siyo kwamba hana furaha.
Kwa mujibu wa Mtandao wa E! News, Kanye West  alisema kuwa mara nyingi akitazama picha za watu wakiwa wamevaa vizuri hugundua hawatabasamu kwa sababu picha zao haziwi poa wakitabasamu.

“Hata picha za wafalme kwenye makasri hawatabasamu kwa sababu picha haiwi kali ukitabasamu. Mapaparazi mara nyingi hunifuata na kuniuliza kuhusu hili lakini nadhani kutotabasamu kwangu kunanifanya nitabasamu,” alisema Kanye West .

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.