Vifaa vya uokoaji ni vitu muhimu katika
jamii hasa pale matatizo yanapotokea, ni vizuri msaada ukapatikana
mapema pale ambapo unahitajika, Serikali ya Kenya imeamua kufanya hili
kama moja ya njia za kuboresha huduma ya dharura kwa watumishi wa umma.
Tumesikia malalamiko mengi kutoka kwa
watumishi wa Serikali kuhusu huduma kuwa si za kuridhisha mbali na kuwa
wanakatwa kodi kubwa kwenye mishahara yao kila mwezi.
Kenya wamezindua huduma za dharura kwa
kutumia ndege na magari ya kisasa kwa watumishi wa umma, uzinduzi wa
huduma hiyo ulihudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Huduma hiyo imezinduliwa kwa ushirikiano
na Shirika la Bima ya Afya, Shirika la Msalaba Mwekundu na kundi la
madaktari wanaosafiri kwa ndege la AMREF.
Huduma hiyo inafanya Kenya kuwa nchi ya
pili baada ya Afrika Kusini kutoa huduma ya aina hii, inatarajiwa kuwa
msaada mkubwa kwa wanajeshi ambao wanapigana vita katika maeneo
mbalimbali yaliyopo mbali na maeneo yenye huduma za afya.
Hapa unaweza kuona namna ambavyo AMREF wameuwa wakifanya shughuli zao za uokoaji.