Mwanaume mmoja nchini Japan ameshtakiwa kwa kosa la mauaji baada ya kujaribu kumuua mwanaye kwa kuweka gari lake kwenye moto wakati mtoto huyo akiwa ndani ili apate muda wa kwenda kujirusha na mkewe.
Polisi wa nchini humo walisema wamemshtaki mwanaume huyo mwenye miaka 71Noriaki Kusaka baada ya kujaribu kuua kwa kukusudia.
Kwa mujibu wa upelelezi wa Polisi tukio hilo lilitokea usiku wa jumapili ambapo polisi walipigiwa simu na kutaarifiwa husu gari hilo kushika moto na kuamua kwenda wakiambata na gari la zima moto.
Mtoto huyo alikutwa na majirani akiwa na hali mbaya baada ya kuungua sehemu kubwa ya mwili wake na kukimbizwa hospitali.