Wanawake wanapokuwa wajawazito huwa na dalili mbalimbali ambazo zinashiria kwamba kuna kiumbe kinatarajiwa kuzaliwa baadaye.
Lakini story ya mwanamke huyu inaweza kukushtua kidogo, alishindwa kufahamu kama ni mjamzito kwa kipindi chote cha miezi tisa.
Katie Kropas akiwa na mwanaye Ellie.
Katie Kropas anayeishi Massachusetts, Marekani alisema alikwenda hospitali baada ya kusumbuliwa na maumivu ya mgongo, alishangazwa na majibu ya madaktari waliompima na kumwambia kuwa vipimo vinaonyesha ni mjamzito na wakati wowote anaweza kujifungua.
Saa moja baada ya kupewa taarifa hizo, mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kike na kumpa jina la Ellie.
“Nilijigundua ni mjamzito baada ya kuja hospotali na saa moja baadaye nikajifungua, nilijihisi uzito umeongezeka lakini sikujua kama ni mjamzito“