Akizungumza na Global TV online kwenye Kipindi cha Mtu Kati, mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Rashid Sultan amefunguka na kuelezea mahusiano yake na mwigizaji Elizabeth Michael ‘lulu’ ambapo Idris alisema amejuana na kuwa marafiki na Lulu kupitia kazi yake ya kupiga picha na kusanifu kurasa za majarida ambayo alikuwa akiifanya.
Swali: Vipi kuhusu uhusiano wako na msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’?
Idris: Mimi ni mpiga picha na msanifu kurasa, Lulu alikuwa anakuja nampiga picha na ni rafiki ambaye tumejuana kwenye kazi tu, sitaki kujua amejiwekaje.
Idris: Mimi ni mpiga picha na msanifu kurasa, Lulu alikuwa anakuja nampiga picha na ni rafiki ambaye tumejuana kwenye kazi tu, sitaki kujua amejiwekaje.
Mbali na hayo, Idris alizungumzia ndoto zake za kufanya kazi Hollywood ambapo alisema anaamimi ana kipaji kikubwa cha kuigiza jampokuwa kwenye jumba alionyesha kipaji cha kucheza.
“Nina ndoto kubwa ya kufika huko, nilivyofika kwenye ile nyumba nilikuwa nina kipaji cha kucheza lakini pia naamini niko vizuri kwenye uigizaji hata kutoka kwa Fig, Big, washiriki wenzangu, mwalimu mwenyewe anashangaa kwa hiyo ninahitaji kuendeleza hicho kitu”-Idris alimaliza.