Mrembo na mwanamitindo ambae pia ni mwigizaji wa filamu na mjasiriamali, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amemrushia maneno makali aliyewahi kuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa hana akili timamu kufuatia maneno aliyotoa kuwa enzi za uhusiano wao, eti mwanadada huyo alikuwa akichenga kumzalia mtoto.
Hivi karibuni akizungumza na Global TV online, Diamond alifunguka: “Jokate na Wema (Sepetu) nilitamani sana wanizalie lakini walikuwa wakichengachenga, mambo mengine ujue si ya kuzungumza lakini inauma.”
Kufuatia tuhuma hizo nzito huku kukiwa na madai pia, kwamba Jokate aliwahi kupigwa mimba ‘akaipanchi’, mwanadada huyo alipotafutwa na mwandishi wetu kujibu ‘shitaka’ linalomkabili alianza kwa kumshangaa Diamond.
Jokate alisema anamshangaa Diamond kuyazungumza maneno hayo hadharani na inaonesha asivyokuwa na akili timamu au ambayo haijakomaa.