Exclusive news ni kwamba Producer Sheddy Clever mmiliki wa Burn Records ndiye atakayehusika katika utengenezaji wa ngoma mbili za msanii wa bongo ambazo amewashirikisha wasanii wakubwa afrika yani kundi la P Square na Mwanadada Tiwa Savage wote wa Nigeria, Sheddy Clever amesema kwa wakati huu hamtaji msanii wa bongo aliyewashirikisha wasanii hao mpaka time itakapofika ya kufunguka hivyo, aidha Sheddy amesema kufanya Collabo hizo kubwa ni matunda ya kufanya kazi na Diamond Platnumz na tayari ameshafanya na Diamond ngoma saba, tatu zimeshatoka ikiwemo Number One, Number Remix ft Davido na Ntampata wapi zote zimefanya vizuri katika level za kimataifa.
Sheddy alimalizia kwa kusema kuwa hajutii ku record bure wimbo wa My Number One wa Diamond, kwani hakuwahi kuota kufanya kazi na P Square au Tiw Savage ila leo kupitia Diamond imewezekana.
msikize Sheddy anafunguka hapo chini...