Friday, January 16, 2015

SPORTS: BERAHINO AFUNGIWA KUENDESHA GARI MIEZI 12

Mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino amepigwa marufuku kuendesha gari kwa kipoindi cha miezi 12 baada ya kukiri kosa la kuendesha gari akiwa amelewa. Berahino, 21 alikamatwa na polisi saa za alfajiri Oktoba mwaka jana. Mahakama ya mwanzo ya North Cheshire mjini Runcorn pia imempiga faini ya pauni 3,400.
Mchezaji huyo ambaye kiwango chake kimekua kiasi cha kuitwa katika kikosi chatimu ya taifa ya England mwezi Novemba, lakini hakucheza katika mechi dhidi ya Slovenia na Scotland.
Berahin, mzaliwa wa Burundi na ambaye alihamia Uingereza akiwa mdogo, alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu na nusu kuichezea West Brom Disemba 2013.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.