Thursday, January 8, 2015

Uzinduzi wa Kitabu cha Marehemu Kanumba Utafanyika Hotel Ya Land Mark Jijini Dar

UZINDUZI wa kitabu cha mwigizaji wa filamu hayati Steven Kanumba unatarajia kuandika historia kufuatia maandalizi yaliyopangwa anasema mratibu wa tamasha hilo Mohamed Mwikongi ‘Frank’ amesema kuwa kutakuwa na mambo muhimu sana kwa ajili ya kumuenzi msanii huyo ambaye aliitangaza Tanzania kimataifa.
“Tumepanga kufanya mambo makubwa kwa ajili ya mwenzetu na tunataka ijengeke tabia ya kuenzi wasanii mbalimbali, pesa za uzinduzi wa kitabu hiki utafungua Kanumba Foundation kwa ajili ya kusaidia wanawake wajane na watoto yatima,”anasema Frank.
Frank anawakaribisha wadau wa Kanumba kwa kufika na kujione kazi za marehemu Kanumba na kuoshuhudia wimbo maalumu wa Marehemu Kanumba utakaoimbwa na mwanamuziki nyota Christian Bella kwa ajili ya tukio maalum .                                 
Kitabu cha historia ya maisha ya mwigizaji nyota Swahilihood Hayati Steven Kanumba kinatarajiwa kuzinduliwa tarehe 10 January 2014 katika ukumbi wa Landmark Ubungo, uzinduzi huo utaambatana na maonyesho ya kazi za marehemu Kanumba alizowahi kushiriki na kuzifanya.
Mama yake mzazi akiongea na waandishi wa habari amewashukru wale wote ambao wamekuwa wakijaribu kufanya kazi ambazo kwa njia moja au nyingine zinamkumbuka mwanaye ambaye aling’ara katika tasnia ya filamu Swahilihood na kufanikiwa kutangaza Tanzania.
“Nawashukru sana watanzania na wale ambao si Watanzania wamekuwa faraja sana kwangu, hasa pale ambapo wamekuwa wakiona umuhimu wa kumuenzi Kanumba kwa njia tofauti tofauti, nawashukru sana, na najua kila mtu ana mchango mkubwa si rahisi kuwataja majina maana mpo wengi,”anasema mama Kanumba.
Kitabu hiki kinachohusu maisha ya Kanumba The Great Fallen Tree kimeandikwa na E. Emmanuel kutoka nchini Canada na kuhaririwa nchini Marekani na kufanyiwa uchapishaji nchini Kenya.
Uzinduzi wa kitabu utasindikizwa na Christian Bella na Bendi ya Malaika kiingilio ni Ths. 20,000/ na utapata kitabu kimoja bure  ukiingia tu mlangoni na kazi zote za Hayati Kanumba zitapatikana siku hiyo.
USIKOSE TUKIO HILI LA AINA YAKE!

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.