Mwigizaji wa filamu Bongo, Wastara Juma amelizungumzia swala la mastaa wengi wa filamu kuto udhuria kisomo cha marehemu mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
Mwishoni mwa wiki iliyopita Wastara aliandaa kisomo cha kumuenzi marehemu Sajuki ambapo dua ilianzia kwenye makaburi ya Kisutu alipozikwa na kumalizika nyumbani kwake maeneo ya Tabata Barakuda jijini Dar. Tukio ambalo lilihudhuriwa na mastaa wachache kutoka kwenye tasnia ya filamu ambapo yeye Wastara hadi sasa yupo na hata marehemu mmewe alikuwa ni mwana tasnia hiyo.
Akizungumza na paparazi wa GPL, kuhusu swala la mastaa kususia kisomo hicho, Wastara alisema;
“Hilo nililijua mapema sababu hawa wasanii wenzangu mambo ya maana hawapendi kabisa, hapa ungewaalika kwenye sherehe yenye pombe wangefika kwa wingi lakini suala la dua wameona tabu sana kuja, nimeshazoea siwezi kulipa kisasi kwa yeyote yule nitajumuika nao kama kawaida japo jambo hili limenikwaza mno.”
Baadhi ya mastaa waliofika katika kisomo hicho ni Davina, Sandra, Vanitha, Frank, Nisha na Mtitu.
Pia Wastara kupitia mitandao ya kijamii aliwahukuru wote,kwakuweka picha hiyo juu na kuandika.
“Naashukuru sana watu hawa na wengine wote tuliokuwa pamoja siku ya leo kwenye dua mungu awazidishie inshallah”
Wastara mara kadhaa amekuwa akisema kamwe kwenye maisha yake hataacha kumlilia Sajuki sababu ndiye mwanaume pekee aliyemuonesha upendo wa kweli na kujivunia thamani yake kama mwanamke anayeishi kwenye ndoa.