Msanii Barnaba aliibiwa Guiter lake mwaka juzi Guiter ambalo alipewa zawadi nchini marekani na Mke wa Rais wa 43 wa Marekani bibie Laura Bush, kwa mujibu wa Barnaba anadai kuna siku alikua amepaki gari maeneo ya kinondoni baadae aliporudi akakuta ameibiwa Guiter na mali zake nyingine zikiwa salama, msanii huyo anadai hamjui aliyemuibia ila anahisi atakua miongoni mwa watu anaofahamiana nao ndio waliotekeleza wizi Gita hilo lenye thamani ya zaidi ya Pound 6000 zaidi ya milioni 12 za kitanzania, Barnaba akaomba kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa gita hilo basi atampatia zawadi yenye thamani kubwa ambayo huyo mtu hajawahi kumiliki maishani mwake, na sababu ya kuahidi zawadi kubwa hivyo anadai mwaka huu atasafiri kwenda kuonana na Mama Laura Bush na Kigogo huyo angependa kumwona Barnaba akiwa na Guiter hilo huku likimletea maendeleo ya kimuziki. Sikiliza You Heard hapo chini ...