Saturday, February 7, 2015

INTERVIEW: RUBBY KIPAJI KIPYA NDANI MUZIKI WA BONGO FLAVA

Sasa hivi kila redio ya kijanja utakayo fungulia huwezi kukosa kuiskia ngoma ya Msanii mpya wa muziki wa kizazi Kipya anayeitwa Rubby, ngoma hiyo inaitwa "Na Yule" unaweza kusikiliza kupitia link ifuatayo https://mkito.com/artist-profile/Ruby/6226 wote walioiskia wanakiri kuwa msanii huyo ana uwezo mkubwa sana wa kuimba, na kwa mtindo wake muziki wa kizazi kipya haujawahi kushuhudia kipaji cha aina hii tangu uanze kuwa rasmi kwa zaidi ya miaka 15, simaanishi kuwa hakuna msanii mkali zaidi ya Rubby, nachotaka kumaanisha hapa Rubby amekuja na kitu cha kipekee kilichopo ndani ya Sauti yake, huyu ni zao la Shindano linalo endeshwa kila mwaka na kituo cha radio cha Clouds fm, Serengeti Fiesta Supa Diva ambapo washiriki kutoka miji mbalimbali hushiriki, na mwaka jana kwenye fainali Rubby ndie aliyeibuka mshindi, Kabla ya mashindano hayo Rubby alikua anafanya muziki wa Gospel kanisani, tazama clip hiyo hapo chini usikie akifunguka usiyajua kuhusu ngoma yake ya kwanza, maisha yake kwa ujumla

                                   

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.