Wema Sepetu amefunguka kuhusu Picha zake alizo post siku mbili zilizopita akionekana ndani ya vazi la Harusi/ shela, Wema amedai kwamba Picha hizo ni za Ndoa yake ya siri iliyofanyika hivi karibuni Bomani na ndoa yake imefungwa ki serikali kwa sababu bwana harusi ambaye hakua tayari kumtaja jina dini yake ni Mkristo wakati yeye Wema ni muislam na ndoa hiyo ilihudhuriwa na idadi ya watu wasiozidi watano, na picha alizo post kwenye mtandao zimepigwa katika hoteli ya Double Tree jijini dar es salaam ambako kulifanyika hafla fupi,
Wema akaendelea kutoboa kuwa wanampango wa kusafiri hivi karibuni huenda ikawa nje ya nchi kwa ajili Honey Moon, Wema ameolewa na mwanaume mwenye umri wa kati si kijana si mzee na hajaolewa ndoa ya mitala, yeye ndiye mke wa kwanza kwa mwanaume huyo, sikiliza interview hiyo hapo chini kati ya Soudy Brown na Wema Sepetu