Monday, May 25, 2015

HATIMAYE KAJALA KASALIMU AMRI KWA WEMA SEPETU NA PETIT MAN

Mahakamani: Siku ambayo Kajala alilipiwa fine ya milioni 12 na kunusurika na kifungo
 Lile beef lililodumu kwa karibu miaka miwili au zaidi kati ya wasanii Bongo Movie Wema Sepetu na Kajala inaonekana limekwisha baada ya Kajala kuandika maneno kuntu kutoka moyoni na kuonesha kujutia hali waliyopitia iliyokua inahusisha vichambo na visasi vya hapa na pale, ikumbukwe kwamba beef la wawili hao inasemekana lilianzia kwa bwana Ck ambae awali alikua ni mpenzi halali wa Wema hadi mwanadada huyo alipoamua kumwacha Ck kutokana na kukolea na Penzi la mpenzi wake waliyekua wamepumzishana enzi hizo Diamond platnumz, ndipo bwana Ck akaamua kutoka na rafiki wa karibu na Wema hapa namzungumzia Kajala Masanja, hivi ndivyo beef lilivyoanza na bahati mbaya kabisa Ck aliamua kwenda kumpokonya Wema baadhi ya mali alizowahi kumhonga, sasa tangu kipindi hiyo Wanadada hao wakawa mahasimu hawapikiki chungu kimoja hata kundi lao kubwa la marafiki liligawanyika vipande viwili na kuanza kurushiana madongo, bila kujali historia yao pande zote zilisahau jinsi walivyofarijiana hasa kipindi ambapo Kajala alikua na msala mahakamani hadi akatupwa Gerezani kwa miezi kibao Wema pamoja na aliyekua mpenzi wake Kajala Petit Man walikua wanahakikisha Kajala anapata mahitaji yote muhimu Gerezani na Wema alienda mbali zaidi kwa kumlipia Kajala Fine ya mamilioni ili asitumikie kifungo baada ya kukutwa na hatia ya kupuuza amri ya mahakama iliyomtaka asiuze mali za mume wake aliyekua ana kesi nzito mahakamani mali ambazo zilikuwa zinachunguzwa iwapo zilipatikana kihalali au La.

Sasa leo katika hali ya kushangaza Kajala ameandika bonge la Ujumbe kwa followers wake wa Instagram, ujumbe ambao ni dhahiri shahiri ameamua kushusha mapanga kwa Wema na Petit Man, usome hapo chini
BINADAMU TULIUMBWA KUISHI KATIKA MISINGI YA UBINADAMU NA SIO UNYAMA KAMA WAISHIVYO WANYAMA WA PORINI LEO NAOMBA KUSEMA KUTOKA MOYONI MWANGU.. NAJUA KABISA NINA WAZAZI WANGU NDUGU ZANGU NA ZAIDI SANA MUNGU WANGU ILA KUNA WATU MPAKA NAKUFA KAMWE SINTOWASAHAU KATIKA KUTA ZA MOYO WANGU KATIKA KIPINDI CHANGU KIGUMU NILICHOPITIA MLIKUWA NEMBO NAMBONI KUBWA KATIKA KUOKOA MAISHA YANGU... NAPENDA KUSEMA KUWA HATA KWA HAYA YOTE TUNAYOPITIA BADO NI MADOGO SANA KUFICHA THAMANI YENU MLIYOIJENGA JUU YANGU..NAKUMBUKA SANA MLIPOJITOA KWA AJILI YANGU MLIPOJINYIMA KWA AJILI YANGU MLIPOPIGANA KWA AJILI YANGU,MLIVYOFEDHEHEKA KWA AJILI YANGU YOTE HAYO NAYAKUMBUKA NA NAMSHUKURUU MUNGU KWANI NAONA KABISA MLILETWA DUNIANI KWA SABABU NYINGI NA MOJA YA SABABU ILIKUWA KUNIOKOA KATIKA KIPINDI KIGUMU KATIKA MAISHA YANGU.LEO HII TAREHE 25.5.2015 NAPENDA KUSEMA KWA UMMA NA ZAIDI KWA MUNGU WANGU KUWA NAWATHAMINI NAWAPENDA NA NASHUKURUUU SANA KWA YOTE MLIYOFANYA JUU YANGU.. NAWAOMBEA KWA MUNGU MUENDELEE NA MOYO HUO HUO KWANI NAAMINI KUNA WENGI BADO WANAWATEGEMEA ILI KUKOMBOA MAISHA YAO KWA WAKATI ALIYOPANGA MUNGU

HATA KITABU CHA DINI KILISEMA KUWA "huwezi kumpenda Mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu yako unayemuona" NAJUA SIKU MOJA TUTAISHI KAMA ZAMANI.. AHSANTENI
Kitendo cha Kajala ni cha kiungwana na anastahili pongezi kwasababu lolote lisilokua na mwisho.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.