Saturday, June 27, 2015

YOU HEARD: JAGUAR AINUNUA KESI YA MSANII ALIYERUKA UKUTA WA IKULU ILI AKAMWOMBE RAIS PESA YA KURECORD WIMBO

Kijana aliyeruka ukuta wa Ikulu Mathew Maina
Kijana Mathew Maina raia wa kenya wiki hii amesimamishwa kizimbani kwa kosa kuruka ukuta wa ikulu ya Rais Uhuru Kenyatta, alipoulizwa sababu za kufanya hivyo kijana huyo akajibu kuwa la yeye ni msanii ila kutokana na ukata unaoikumba familia yao hawezi kugharamia malipo ya kurecord wimbo studio na hivyo aliamua kuruka ukuta huo ili aonane uso kwa uso na rais kenyatta kisha amwombe msaada huo, lakini kwa bahati mbaya alishindwa kutimiza ndoto yake na kuishia mikononi mwa wana usalama waliomkabidhisha kwa polisi na hatimaye akajikuta mahakamani, Mahakama hiyo ikaamuru kwamba kijana huyo akapimwe akili kisha hatua zingine zifate, na kwa wakati huu kijana Mathew Maina yuko rumande.

Wakati huohuo Msanii Jaguar amejitolea kumsaidia kijana huyo kwa kumlipia gharama za studio, na pia ameamua kumtembelea Gerezani ili kusikiliza majanga yake na kuangalia kama kuna uwezekano wa kumdhamini.ki
sikiliza mahojiano kati ya Mtangazaji Soudy Brown na Ms.anii Jaguar wa Kenya

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.