Tuesday, June 23, 2015

SUGU ASHINDA KESI DHIDI YA MAMA WA MTOTO WAKE (FAIZA ALLY)



Kesi ya kudai mtoto iliyofunguliwa na mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu dhidi ya mama wa mtoto wake Faiza Ally imetolewa hukumu leo katika Mahakama ya Mwanzo Sinza Mori, Kesi hiyo ilianza kusikilizwa wiki iliyopita ambapo mbunge huyo alidai kwamba ana wasiwasi na malezi ya mwanae Sasha kutokana na kulelewa na mama yake bila maadili, mbunge huyo aliwasilisha vielelezo vya picha vya mama wa mtoto huyo akiwa amevalia nguo ya kuogelea pamoja na ya mtoto pia aliwasilisha picha ya mwanadada huyo akiwa na ile nguo aliyovaa kwenye Red Carpet ya Kili Tanzania Music  Awards (KTMA)
katika Utetezi wake Faiza alitoboa  kuwa eti mbunge huyo hawezi malezi na kazi zake nyingi ni za kusafiri kama mbunge, pia eti mbunge huyo anapuliza sana na kunywa pombe kupita maelezo,
mahakama hiyo iliskiliza pande zote na kumuamuru Faiza ampe mtoto Sugu amlee, hali iliyomuacha mwanadada huyo katika majonzi mazito na kilio,
Nimefanikiwa kuzungumza na Faiza Live bila chenga, mambo yamemfika Hapaaaaa, mskilize hapo chini...............

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.