Tuesday, August 30, 2016

Mzee Majuto Na Wema Sepetu Hii Movie Iliishia Wapi?

Mzee Majuto Na Wema Sepetu.
Takribani miaka miwili sasa tangu tuliposikia huenda ikafanyika movie kati ya mastaa Wema Sepetu pamoja na mkali wa vichekesho Afrika Mashariki "King Majuto" ambayo pia ingemuhusisha mbongoflava Diamond Platnumz ambae alikua mpenzi wa Wema Sepetu Enzi hizo.
Diamond Platnumz Na Mzee Majuto.
Kwenye moja ya interview zake Mzee Majuto aliwahi kukaliliwa kuwa huenda movie hiyo ingefanyika kana alivyonukuliwa hapa     “Hivi karibuni nilikuwa na Wema, nimemwambia aongee na Diamond ili tufanye filamu ya pamoja,” amesema Majuto. “Mimi, Wema na Diamond, hata Diamond ninaweza kuzungumza naye sema nimeanza na Wema kwanza, akikubali mtasikia tu.”.a
Macho na masikio ya wapenzi wengi wa burudani yalielekezwa kwa mastaa hawa watatu huku kila mmoja akiwa na mtazamo wake jinsi movie hiyo ambavyo ingekua.
 Mpaka sasa ni muda umepita na hatusikii chochote kuhusu hilo au ni tofauti zilijitokeza katikati ya zilipendwa hao ndio zilipeleke kuahirishwa kwa zoezi hilo?aele  M


ANGALIA HII YA MZEE MAJUTO AKICHEZA KUNG-FU

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.