Showing posts with label Diamond Platnumz. Show all posts
Showing posts with label Diamond Platnumz. Show all posts

Thursday, October 13, 2016

Misaada aliyopewa Said Ally alietobolewa macho na 'Scopion' Buguruni,Dar es salaam.




Said Ally Mrisho alielezea mkasa mzima kupitia mahojiano aliyofanya na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM ambapo watu mbalimbali wameweza kumchangia fedha na vitu vya kumsaidia kuendesha maisha yake,hasa kumuingizia kipato kwani kwa sasa hawezi tena kufanya shughuli zake za kila siku baada ya kutobolewa macho na mtu anaefahamika kama 'Scopion' mapema mwezi uliopita eneo la Buguruni Jijini Dar es salaam.

Miongoni mwa misaada aliyopoke ni pamoja na TZS milioni 10 ambazo amepewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salam,Paul Makonda aliedai kuwa yupo kwa ajili ya kusaidia wanyonge na wenye mahitaji kama alivyoagizwa na Rais Magufuli huku akiahidi kumlipia gharama za elimu ya wasioona ili  aweze kuwasiliana kwa njia ya alama ikiwa ni pamoja na kumnunulia fimbo maalumu ya kumsaidia kutembelea.


Mbali na Mkuu wa Mkoa,Said amepewa msaada wa pikipiki 5 ambapo kati ya hizo,2 ni msaada kutoka kampuni ya Infotech na 3 zikiwa ni msaada kutoka TSN.Pia ndugu Admjee amemsaidia Said Bajaji 2 ambapo vyote hivi vimepatikana kutokana na juhudi za RC,Makonda kutafuta watu wa kumsaidia bwana Said.

Kwa upande mwingine GSM kupitia ushawishi wa Mkuu wa Mkoa imesema kuwa itamnunulia  Said nyumba ya kuishi ambapo baada ya kushukuru alilizwa angependa nyumba hiyo inunuliwe maeneo gani na Said alipendekeza nyumba hiyo iwepo eneo la Tabata,Dar es salam kwani ndilo eneo alilolizoea kutokana na kuishi hapo tangu mwaka 1999.


Kwa upande mwigine Mwanamuziki Diamond Platnumz amejitolea msaada wa TZS milioni 2 hii ikiwa ni baada ya Said kwenye mahojiano yake kudai kuwa moja ya vitu alivyo-miss kuvitazama ni pamoja na video ya wimbo 'Salome' wa Diamond Pltnumz,hali iliyomlazimu Mwanamuziki huyo kufika Clouds fm kutoa msaada huo.

Said Ally amabae ni baba wa familia ya watoto 5,kabla ya kukubwa na mkasa huo wa kutobolewa macho na mtuhumiwa "Scopion",alikua akifanya ya kinyozi maeneo ya Tabata.

Mtuhumiwa 'Scopion',anaedaiwa kumtoboa macho Said anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi na tayari amefikishwa mahakamani na kusomewa mashataka yanayomkabili ili haki iweze kupatikana.


Wednesday, October 12, 2016

VIDEO:Waziri January Makamba atembelea studio ya Diamond Platnumz,(WCB).



Mbunge wa Bumbuli na Waziri wa nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia muungano na mazingira,January Makamba,October 12,alifanya ziara kwenye ofisi za lebo ya muziki ya WASAFI (WCB),inayomilikiwa na Mwanamuziki Diamond Platnumz.

Sio jambo la kushangaza kwa Waziri huyo kutembelea studio hizo kwani licha ya kupata bahati ya kuteuliwa kwenye nafasi kadhaa za uongozi nchini,amekua mtu wa kujichanganya na kushiriki shughuli za makundi mbalimbali  ya kijamii hasa vijana.

Katika mchakato wa Urais kupitia chama chake (CCM) mnamo mwaka 2015,aliingia kwenye tano bora ya wagombea waliopendekezwa kugombea urais kwa tiketi ya chama chake,na kuwa kijana pekee aliewatoa kimasomaso vijana wa chama hicho kwenye nafasi hiyo nyeti ya uongozi.

Thursday, October 6, 2016

Diamond amtetea Mama yake kwa kuto-post picha ya Zari.


Katika mahojiano aliyofanya kituo cha redio cha Times Fm,Diamond Platnumz aliulizwa kwanini mama yake hakuweka mtandaoni picha ya Zari wakati akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa lakini aliweka picha ya Wema Sepetu alipokua akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa na kama ni kweli kuwa kuna ugomvi kati Mama yake na Zari,Diamond alisema haya.

"Sisi ndio pambo la mitandao,Mtu akiamka lazima aingie kwenye familia ya kina Diamond ajue inafanya nini,ni familia ambayo ina mashikamano na ipo kibiashara zaidi".

"Inabidi tuwape watu vitu vya kuzungumza zaidi,Kila kinachofanyika kinafanyika kwa makusudi na Mama yangu na Zari wanaelewana sana,ndio maana Zari yupo Tanzania kwa sasa".

Saturday, October 1, 2016

Utapenda Majibu Ya Mondi Kuhusu Kiba Na MTVEMA

 http://thedouglasreview.com/wp-content/uploads/2016/04/Diamond-Platnumz.png
 Diamond Platnumz amewataka mashabiki zake wampigie kura msanii Alikiba kwenye tuzo za MTV EMA akiwa kama msanii pekee kutoka Tanzania aliyechaguliwa kuwania tuzo hizo.
Licha ya tofauti ambazo inasemekana wawili hao wanazo, mkali huyo amewataka mashabiki wake waweke mambo ya u-team pembeni na wajikite kwenye kuliletea taifa faida.
Akihojiwa kwenye kipindi cha D’Wikend Chatshow kinachoruka Cluds TV Ijumaa saa 3 usiku Diamond Platnumz alidai kuwa yeye binafsi hana tatizo na Alikiba ndio maana habari za tofauti zao zinazidi kupungua siku hadi siku, na kama angekuwa na tatizo nae kweli basi ingejulikana wazi kwasababu yeye bifu lake huwa haliishi na wala sio la kujificha.
“Nimesikia Alikiba amechaguliwa kwenye tuzo za MTV EMA, tufute zile zama za kusema kwasababu wewe unamsapoti Diamond ndio huwezi kumpigia kura Alikiba, kwasababu yeye akikosa tuzo hiyo haiji kabisa Tanzania na itaonekana watanzania wote tumeikosa. Kwahiyo tuhakikishe tuna VOTE ili tuirudishe tuzo hiyo nyumbani.” Alisema Diamond Platnumz.

Thursday, September 22, 2016

VIDEO:Diamond amrudisha Wema Sepetu kwa Idris Sultan kiaina.



Wakati kasheshe la kukutwa kwa hereni ya Mwanamke chumbani kwa Mama watoto wake Zari The Boss Lady likiendelea kufukuta,Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond amepost video ya aliekua X-Girl wake Madam Wema Sepetu akiimba wimbo wake mpya "Salome" na kuandika ujumbe ambao baadhi ya mashabiki wanahisi Diamond anajaribu kulirudisha penzi kati ya Mshindi wa BBA-2015 Idirs Sultan na Wema Sepetu ambao mapenzi yao yanadaiwa kuyeyuka tangu mwanzoni mwa mwezi July Mwaka huu.


"Hivi huku patakuwa ni kupatwa kwa nini....??? Tisha sana #SALOME wake @idrissultan full Video link in my BIO and @rayvanny BIO☝.....Shukran sana".Ameandika Diamond.


 Hizi ni baadhi ya coment za mashabiki;
 

Saida Karoli ameandika haya Instagram kwenda kwa Diamond Platnumz.


Jumapili ya wikend iliyopita Diamond Platnumz aliachia wimbo mpya "Salome" akimshirikisha msanii ambae yupo chini ya lebo yake ya WCB,Ray Vany ambapo awali wimbo huu uliimbwa na Mwanamuziki wa nyimbo za asili Saida Karoli ambapo kwa wakati hit's hiyo inatoka  kwa mara ya kwanza mwaka 2001 ulifahamika kama "Maria Salome".


Kupitia ukurasa wake wa Instagram Saida Karoli ame-post ujumbe huu kwenda kwa Diamond Platnumz ambae uongozi wake ulifikia makubaliono ya kurudiwa kwa wimbo huo ambao ndani ya siku mbili tangu video yake ilipotoka imefikisha watazamaji milioni 1.


"Ahsante sana mdogo wngu kwa zawadi hii Mungu akujalie uzidi peperusha bendera ya nchi yetu nimefurahi sana".Ulisomeka ujumbe huo.




PICHA:Mwenye hereni iliyokutwa chumbani kwa Diamond abainika.

 Mama watoto wa Mwanamuziki Diamond Platnumz,Zari The Boss Lady ameendele kutupa madongo kwa wanawake anaohisi wanatoka kimapenzi na Diamond baada ya kupost video kupitia mtandao wa "Snapchart" akiandika ujumbe kwenda kwa mwanamke anaedai ameacha hereni kwenye moja ya vyumba vyake bila kumtaja jina.

 Kupitia mitandao ya kijamii kumwekua na picha inayosambaa ikionesha picha ya hereni inayodaiwa kukutwa kwenye moja ya vyumba vya nyumba ya Diamond,Madale Tegeta huku upande wa pili ikionekana sura ya Mwanamitindo Hamisa Mabeto ambae hereni aliyovaa katika picha hiyo inafanana na hereni iliyozua kasheshe.






  Posts hizo za Zari zinaendelea kukuza tetesi za muda mrefu juu ya  usaliti kwenye  mahusiano yake w na Diamond hivyo pengine Mwanamama huyu ambae ana ujauzito wa pili kwa Hit maker wa singo ya "Kidogo",ameamua kuchukulia poa kuivumilia tabia ya Diamond japo suala hili linaweza kuchafua hali hewa kwenye mahusiano ya mastaa hawa.
Ikumbukwe kuwa kwa muda sasa Mwanamitindo Hamisa Mabeto amekua akiandamwa na skendo ya ku-share kitanda na Diamond ambae amekua akikanusha madai hayo,ambapo hata hivyo Mwanamuziki huyo amekuza tetesi hizo mara baada ya Hamisa kuonekena kama "Video Queen" kwenye video ya wimbo mpya wa Diamond aliomshirikisha Ray Vany unaofahamika kama "Salome"




Tuesday, September 20, 2016

Picha | Angalia Mashabiki Wanavyotoleana Mapovu Kuhusu Salome

Usiku wa septemba 18 wanamuziki Diamond Platnumz na Rayvanny waliachia ngoma ya kwanza tangu kuungana kwao kwenye label WCB.

 Haikua kuachia ngoma tu bali ilikua ni kuvunja rekodi ya muziki wa Afrika kwani tangu kuachiwa kwake hapo Juzi "Salome" imekua habari ya mjini,

 Wimbo "Salome" uliimbwa na mwanamama Saida Karoli katika vionjo na  Tamaduni za kabila la Kihaya umerudiwa na Diamond Platnumz pamoja na Rayvanny umeendelea kuwa gumzo kwani katika hali isiyokua ya kawaida mashabiki wameendelea kusifu huku wengine wakitoleana mapovu kuhusu Diamond Kuirudia Ngoma hiyo.

ANGALIA BAADHI YA COMMENT ZA MASHABIKI: 




Video ya Salome huenda ikatajwa kuwa video ya Kiafrika iliyotzamwa mara nyingi ndani ya muda mfupi kwani tangu kuwekwa kwake kwenye mtandao wa YouTube siku mbili zilizopita tayari imeangaliwa zaidi ya mara Laki sita.

Monday, September 19, 2016

Video:"Salome",Diamond Platnumz ft.Ray Vany.


Msanii Diamond Platnumz ameamua kuachia video mpya ya wimbo ‘Salome’ amemshirikisha Rayvanny, Video imefanyika hapahapa Tanzania, imeongozwa na Director Nicorux kutoka South Africa.


 

Sunday, September 11, 2016

"Nyaku Nyaku's"ajitokeza,amwita Zari bibi kizee.



Baada ya mama watoto wa Mwanamuziki Diamond Platnumz,Zari kupost picha akiwa na Diamond na kutuma ujumbe kwa wanawake wanaotajwa kuchepuka na mwanamuziki huyo akiwaita "Nyaku Nyaku''s" kwa madai kuwa hawana ujasiri wa kuwaweka wapenzi wao hadharani,Hataimae amejibiwa na Mwanamitindo na Video Vixen kutoka nchini Kenya,Hudda Monroe alieenda mbali  kwa kumuita bibi na kuongeza kuwa Mwanamama huyo anaedaiwa kuwa na ujauzito wa pili kwa Diamond anatafuta kiki.


                                                      Hudda Monroe.

Kwa muda sasa mitandaoni kuwemo na taarifa za Diamond kutoka kimapenzi na warembo wengine huku Mwanamitindo Hamisa Mabeto akiwa miongoni mwa wanamitindo wanaotajwa ku-share kitanda na hit maker wa singo ya "Kidogo",hivyo huenda majibizano haya ya mitandaoni yakaibua mengi tusiyoyajua.

Friday, September 9, 2016

Diamond Platnumz Na Kelvin Hart Wajikuta Ni Mapacha Wa Roho.



Kelvin hart amezaliwa mwaka 1979
Diamond amezaliwa mwaka 1989 kwa hyo kuna tisa tisa hapo
kevin hart anatokea philadelfia pennyslyvania uswaz sehem ambako kunasifika kuwa na ma gang mengi ya uhalifu
diamond platnumz anatokea uswaz tandale sifa zake zinafanana na alikotokea kevin hert
kevin hart amelelewa na mama yake kwa karibu,
diamond pia amelelewa na bi mdanga wake kwa karibu sana bi sandra
kevin hart ktk hussle zake amewahi kuuza duka la viatu
diamond pia ktk hussle zake alikua anauza mitumba ya viatu
kevin hart amewahi kuzomewa mara kadhaa kwenye majukwaa hadi kuna siku alirushiwa kipande cha kukuu, madharau
diamond amewahi kuzomewa jukwani akarushiwa mayai viza maisha club
kevin hart ana watoto wawili
diamond ameshatangaza kuwa anatarajia mtoto wa kiume kutoka kwa zari
kevin hart alianza kutoboa mainstream na comedy mwaka 2009
diamond nae alitoka na kwamwambie mwaka 2008 2009

Thursday, September 8, 2016

Diamond,Ali Kiba na Ya Moto Band watajwa kuwania tuzo za Afrima.

Tuzo za Afrima zinazoandaliwa kwa ufadhili wa taasisi ya African Union Commission (AUC)     zimetangazwa huku orodha kamili ya wasanii wanaowania tuzo ikimjumuisha Msanii wa Bongo Fleva,
Diamond anaewania vipengele vitano.

Viepengele hivyo ni pamoja na  Songwriter of The Year in Africa, Song of The Year in Africa, Artiste of The Year, Best Artist in Africa na Best Male Artist in Eastern Africa.

Watanzania wengine waliotajwa kwenye tuzo hizo ni pamoja na Alikiba anayewania cha Best Male Artist in Eastern Africa na Yamoto Band likitajwa kuwania kipengele cha Revelation of The Year.
Tazama orodha kamili,


 afrima



afrima1

afrima2

afrima4
afrima5afrima4afrima6afrima3


afrima8
 afrima9

Thursday, September 1, 2016

VIDEO:Diamond Platnumz uso kwa uso na Kevin Hart.


Diamond Platnum amekutana na mchekeshaji huyo maarufu ulimwenguni kwenye ziara yake nchini Marekani ambapo amekua akishoot video ya wimbo wake mmpya "Marry You" aliomshirikisha mkali wa miondoko ya RnB Ne-Yo.

                                             Mchekeshaji  Kevin Hart.


A video posted by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on


Baadhi ya picha wakati wa kurekodiwa kwa video ya Diamond & Ne-Yo ijini Los Angeles nchini Marekani.

14052200_1779586832299906_318731167_n




14099274_652267324950266_798681766_n








14031609_171648116595722_1232327386_n
 14026554_1450796224937406_1965298587_n

Tuesday, August 30, 2016

Mzee Majuto Na Wema Sepetu Hii Movie Iliishia Wapi?

Mzee Majuto Na Wema Sepetu.
Takribani miaka miwili sasa tangu tuliposikia huenda ikafanyika movie kati ya mastaa Wema Sepetu pamoja na mkali wa vichekesho Afrika Mashariki "King Majuto" ambayo pia ingemuhusisha mbongoflava Diamond Platnumz ambae alikua mpenzi wa Wema Sepetu Enzi hizo.
Diamond Platnumz Na Mzee Majuto.
Kwenye moja ya interview zake Mzee Majuto aliwahi kukaliliwa kuwa huenda movie hiyo ingefanyika kana alivyonukuliwa hapa     “Hivi karibuni nilikuwa na Wema, nimemwambia aongee na Diamond ili tufanye filamu ya pamoja,” amesema Majuto. “Mimi, Wema na Diamond, hata Diamond ninaweza kuzungumza naye sema nimeanza na Wema kwanza, akikubali mtasikia tu.”.a
Macho na masikio ya wapenzi wengi wa burudani yalielekezwa kwa mastaa hawa watatu huku kila mmoja akiwa na mtazamo wake jinsi movie hiyo ambavyo ingekua.
 Mpaka sasa ni muda umepita na hatusikii chochote kuhusu hilo au ni tofauti zilijitokeza katikati ya zilipendwa hao ndio zilipeleke kuahirishwa kwa zoezi hilo?aele  M


ANGALIA HII YA MZEE MAJUTO AKICHEZA KUNG-FU

Thursday, August 18, 2016

DIAMOND PLATNUMZ AFUNGUKA BAADA YA UBUYU JUU YA KU #KWICHIKWICHI NA WEMA SEPETU


TAKRIBANI MWEZI MMOJA NA NUSU SASA KUMEKUWEPO NA UBUYU WA JUU YA KURUDISHWA KWA MAHUSIANO YA W NA D, WIKI ZA HIVI KARIBUNI UBUYU HUO UKAZIDI KUWA MTAMU KUTOKANA NA WAWILI HAO KUJA NA UTARATIBU WA KUPOSTIANA (MA MCM VEPEEE) KWENYE MITANDAO KIASI CHA KWAMBA HADI WANACHAMA WAANDAMIZI WA KAMBI ZAO NAO KUONEKANA WAKIWA PAMOJA
.
SHIRIKA LA WAMBEA DUNIANI LIKAINGIA MZIGONI NA KUMTAFUTA DIAMOND KUPITIA SIMU YAKE YA MKONONI, MAZUNGUMZO KATI YA D NA MWAKILISHI WA #SHILAWADU NDUGU SOUDYBROWN YALIKUA HIVI, NANUKUU
.
SOUDYBROWN: HALLO
.
DIAMOND: HALLO, NANI?
.
SOUDYBROWN: NDUGU YAKO HAPA GOSSIP COP
.
DIAMOND: OHOO KUMBE WE MBEAA, DAH😨😨... EHE KUNA NINI TENA HUKO MAANA NIPO MAZOEZINI (kauli ya Kujihami)
.
SOUDYBROWN: HAMNA KITU NIMEKUPIGIA KUKUSALIMIA TU 😁
.
DIAMOND: SIDHANI
.
SOUDYBROWN: KWENU MNA ASILI YA NDOA ZA MITALA?
.
DIAMOND: OFCOZ MBONA NINAO NDUGU WANA WAKE WAWILI WAWILI, MI SI MUISLAM RUKSA
.
SOUDYBROWN: HIVI KATI YA ZARI NA WEMA UNAMCHAGUA NANI?
.
DIAMOND: NAMCHAGUA NANI KI VIPI?
.
SOUDYBROWN: KWICHI KWICHI
.
DIAMOND: SOUDY NIPO MAZOEZINI, TUONGEE BAADAE
.
SOUDYBROWN: NASKIA WEMA ANAKUJAGA KUBINJUKA KWAKO CKU HIZI, CKU NYINGINE MADALE CKU NYINGINE PALE PALE WCB 🙈
.
DIAMOND: NANI AMEKUAMBIA? 😨
.
SOUDYBROWN: KATI YA ZARI NA WEMA UNAAAAA.... NANI?
.
DIAMOND: SORRY NTAKUCHEKI BAADAE KUNA MAZOEZI HUKU
.
AKA KATA SIMU FASTA
.
JAMANI YANI KASHINDWAJE KUJIBU KIJISWALI HIKI?
KUNAYO NAMNA 🙈🙈
.
Post kwa niaba ya Shirika la Wambea Duniani
.
Mi simoooooo
.
@Shilawadu #Hatushindwi

 

ANGALIA HAPA VIDEO MPYA YA SAMATA A- KODO



You Heard | Wema Sepetu Kuhusu Kurudiana Na Diamond, Bifu Na Zari Je?

Penzi la mwendokasi limeri-potiwa kuzinduliwa upya mara baada ya zilipendwa Sepenga na Mondi kuonekana kunyemeleana kiaina,
 Sasa basi Gossip Cop +SOUDY BROWN  ameona ubuyu usikupite amemvutia waya madame Wema Sepetu na alikuwa na haya ya kufunguka.

Bonyeza Hapa Kumsikiliza Wema Sepetu.






ANGALIA HAPA KICHUPA CHA SAMATA A - KODO





Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.