Tuesday, September 13, 2016

Kama Wewe Ni Shabiki Wa Future Chukua Hii?




Huenda ukamsikia tena Future kwenye chati kubwa za muziki duniani mara tu atakapoachia project yake “Beast Mode 16” ambayo tayari imekamilika, Kwa mujibu wa Producer Zaytoven ambae ameiambia XXL MAGAZINE ilibidi amkazie mnyamwezi Future kuendelea kurekodi kwani mshikaji bado  na hits kibao.

“Nilikua Na Future kama wiki tatu zilizopita akaniambia anatamani sana kuendelea kurekodi ngoma mpya, ‘natamani niendelee kuingiza vitu vipya lakini kwa hapa tulipofikia acha nifurahishe mashabiki wangu kwani kwa hizi ngoma nilizorekodi zinatosha kabisa kuanza kuziachia ninajivunia sana kuifanya kazi hii na wewe na ninaheshimu maamuzi yako”  Future alimuambia Producer Zaytoven.

Zaytoven  alitangaza ujio wa project hiyo mapema mwezi wa sita ambayo kutokana na sababu zilizokua nje ya uwezo wao yeye na Future hawakuweza kufanikiwa kuiachia kwa kipindi kile amewataka mashabiki wa Future kujiandaa kuipokea Beast Mode 16 kwani ni zaidi ya mixtape.

"Tumemaliza Beast Mode 16, nasikitika kuwaambia kuwa haitokua mixtape" (akiwa na maana itakua ni single release kwa ngoma zote ambazo future amerekodi.)


ULIIONA HII YA MPOKI AKIMFUTA BARAKA DA PRINCE UANACHAMA WA CHAMA CHA WATU WEUSI?



Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.