Wednesday, September 14, 2016

Mh.Zitto Kabwe amtolea povu Waziri Mkuu baada ya kuchangisha michango kwa ajili ya wahanga wa tetemeko.


Mapema jana Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa kukusanya jumla ya kiasi cha takriban shilingi bilioni 1.4 pamoja na vifaa vya ujenzi katika hafla aliyoongoza ya uchangiaji fedha kwa ajili ya waathrika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera katika hafla iliyohudhuriwa na jumuiya ya wafanyabiashara nchini, mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini pamoja na watu binafsi Jijini Dar es Salaam.


Mara baada ya hafla hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa facebook,kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe alitoa mtazamo wake juu ushiriki wa wafanyabiashara katika uchangiaji wa shughuli za serikali.

"Nampongeza sana Waziri Mkuu Kwa Kazi kubwa aliyofanya kuwezesha na kuratibu michango kusaidia maafa huko Kagera. Ninaamini Michango ingekuwa Mingi zaidi iwapo Serikali ingekuwa imeweka mazingira bora zaidi ya watu kufanya Biashara. Bahati mbaya sana Kwa Serikali hii Sekta Binafsi inaminywa sana na hivyo kudororesha Uchumi. Serikali ijifunze kuwa Kazi ya Serikali sio kukusanya kodi tu".Aliandika Mh.Zitto.


 Katika hafla hiyo,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema watanzania 17 wamefariki, majeruhi wamefikia 253 na wagonjwa 143 wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Kagera,nyumba 840 zimeanguka na zingine 1,264 zimeharibika na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na kuitaka kamati ya maafa kupitia maeneo yote ambayo yameathiriwa na tetemeko hilo ili kuhakiki uharibifu uliotokea ili kutoa msaada wa hali na mali kwa walengwa.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.