Thursday, September 15, 2016

Michepuko Yadaiwa Kumponza Kidoa, Nusura Bwana'ake Ampige Chini.

Malikia wa vichupa vya muziki wa bongoflava na mshindi wa Tuzo ya Ijumaa Sexiest Girl Kidoa Salum amenusurika kupigwa kibuti na jamaa yake ambaye anatajwa kuwa kigogo baada ya kufumaniwa kwa meseji za wanaume wengine kwenye simu yake.

 Kwa mujibu wa chanzo chetu, tangu Kidoa ameanzisha uhusiano na kigogo huyo, ameonekana ni mtu mpole na hata mambo ya starehe ameyaweka pembeni lakini kitendo cha kufumwa meseji kimeharibu kila kitu:

“Sasa unaambiwa juzi, Sikukuu ya Idd wakati yupo kwenye mtoko na mpenzi wake huyo, muda wote Kidoa alikuwa bize akichati na mwanaume mwingine jamaa akashtukia mchezo na kumpokonya simu, acha kinuke,” kilisema chanzo.
Kidoa alipoulizwa na mapaparazi wetu alikana ishu hiyo kutokea ambapo alisema siku hiyo hakutoka nyumbani kwao.

SOURCE:GPL 


Kolabo Ya Baraka Na Alikiba Yamchanganya Petitman





Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.