Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza waombolezaji kuaga miili ya waliokufa kwenye tetemeko la ardhi mjini Bukoba,zoezi litakalo fanyika kwenye uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.
Mamia ya wananchi wamekua wakiongozana kuelekea kwenye uwanja huo kuwaaga wapendwa wao ambapo hadi usiku wa kuamkia leo takribani watu 14 wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya 200 wakiathirika na tetemeko hilo lililokua na ukubwa wa (magnitude) 5.7 lililotokea mnamo jumamosi hii na kusababisha maafa katika mikoa ya Mwanza, Kagera na sehemu za Shinyanga.
Source:Mwananchi