Kocha wa Manchester United,Jose Mourinho amewalaumu wachezaji wake akidai kuwa wao
ndiyo sababu ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya mahasimu wao Manchester
City kwa mabao 2-1.
Jose Mourinho.
Man United walijikuta wakipotezwa kabisa na vijana hao wa Pep
Guardiola kwenye dimba lao la Old Trafford, na kujikuta wakiruhusu
magoli mawili yaliyofungwa na Kevin De Bruyne na Kelechi Iheanacho.
Baada ya mchezo huo Mourinho alisema: "Wakati mwingine wachezaji huwavunja moyo mameneja wao".Alimwambia ripota wa Sky Sports. “Kipindi cha kwanza walikuwa vizuri zaidi yetu"....."Tulianza mchezo huku baadhi ya wachezaji wakicheza chini ya kiwango
chao cha kawaida kuanzia kwenye suala la umakini mpaka kasi ya mchezo".
Jose Mourinho (L) na Meneja wa Man-City,Pep Guardiola wakati wa mchezo.
"Unahitaji kuwa na maamuzi ya haraka namna unavyocheza na unavyofikiri"..."Mchezaji mmoja au wawili hivi walikuwa hawapo kwenye kiwango kizuri na hali hiyo imeigharimu timu".Aliongeza Kocha huyo mwenye tambo nyingi.
Mourinho aliwaanzisha Jesse Lingard na Henrikh Mkhitaryan kwenye
kikosi cha kwanza lakini aliwatoa wote baada ya kipindi cha kwanza
kuisha baada ya kuonesha kiwango kisichoridhisha