"Bounce that sh*t like waoh...".Anasikika rapper Drake akiimba baada ya drama fupi inayoonekana kwenye video hii mpya ya wimbo wake unaoitwa "Child's Play" ikiwa ni video nyingine kutoka kweye album yake ya nne "Views" iliyopata mafanikio makubwa kimauzo.
Drake.
Video hii ya dakika 12 ambayo imeongozwa na Drake mwenyewe akishirikiana na Spiff Tv,imemjumuisha mrembo Tyra Banks ambae kwenye video hii amecheza kama girlfriend wa Drake.Drama inaanza hivi,Drake na girlfriend wake wametoka out,wakati wakisubiri mhudumu awaletee "Cheesecake",Drake anaenda maliwatoni,na Tyra anatumia mwanya huo kupekua simu ya Drake na kukuta meseji za mwanamke mwingine anaeonekana kuchepuka na Drizy,jamaa anaporudi girlfriend wake anambadilikia na kwa kumpa makavu live kama watoto wa mjini wanavyosema,tena bila kujali watu kibao waliowazunguka “I am tired of you, Aubrey,”. Anasikika Tyra Banks akifoka. then anammwagia Drake chakula na glass ya wine kichwani kisha na kuondoka.
Nisikumalizie utamu,video hii hapa