Jengo la hoteli linalofahamika kama "Grande Hotel",ambalo zamani lilifahamika kama "Fahari ya Afrika" lipo katika mji wa Beira pwani ya Msumbiji likiwa ni makazi ya jumla ya watu 3,500.
Hoteli hii ilipozinduliwa mwaka 1955,ilitajwa kama miongoni mwa Hoteli za kifahari zaidi barani Afika.Jengo hili la ghrofa 3 lina ngazi refu zinazounganisha shemu ya maduka,migahawa,maduka,jumba la sinema,ofisi ya Posta,vyumba 122 na bwawa la kuogelea ambalo kwa sasa limeuzwa shemu ya kufulia nguo.
Hoteli hii ilifungwa rasmi mwaka 1963 ambapo kutokana na machufuko ya kisiasa jengo hili halikuwavutia wawekezaji licha ya kuwa pembezoni mwa fukwe za bahari ya Hindi.Inadaiwa wakati wa miaka 70's jengo hili lilitumika kama kambi ya jeshi na gereza kwa wafungwa wa kisiasa.
Hata hivyo mara baada ya vita kumalizika jengo hili liliporwa na watu masikini hasa wahanga wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo kwa sasa jengo hili limejaa watu wanaoishi kila kona ya jengo hilo ambapo baadhi yao wamekuwemo kwenye jengo kwa zaidi ya miongo mitatu sasa huku wakikabiliwa na hali duni ya maisha.
Wakazi wanaoishi katika jengo hili hawalipi kodi ila serikali imeweka sheria ya kuzuia wakazi wapya kuishi ndani ya jengo hili kutokana Hoteli kujaa.
Wananchi wanaishi katika Hoteli hii wamejiwekea utaratibu wa kuchagua viongozi wanaoratibu shughuli mbalimbali za kijamii ndani ya jengo hili.
Hizi ni baadhi ya picha za jengo hilo;