Kundi la East Cost lililokua likiundwa na rappers wakali kama King Crazy-GK,AY,Mwana FA,Buff G,Snare na wengine wengi lilitikisa anga ya muziki kati ya mwaka 2003 hadi 2007 kabla kundi hilo kumeguka vipande vipande ambapo AY na Mwana Fa walijitoa na kuuanza ku-release kazi zao nnje ya kundi hilo ambalo lilibaki mikononi mwa GK.
Mwana FA.
Ni muongo mmoja sasa tangu East Cost imeguke ila mapema mwezi huu rapper King Crazy-GK amerudi kwenye game ya muziki kwa kuachia wimbo na video mpya ya wimbo wake unaofahamika kama "Mzuri Pesa".
Kupitia akaunti yake ya Facebook,Mwana Fa amemtania GK kutokana na aina mpya ya muziki alioamua kufanya kwa kupost "Cover" ya wimbo huo na kuandika ..."Ngoja ngoja..masihara kando na ni kwa sababu zifuatazo;..hardcore lina instagram account ambayo ni @kingcrazy_gk makofi tafadhali..lina wimbo wa kuimba narudia haljarapa limeimba hilo hardcore...makofi tena jamani....hardcore hili lina video kali sana kwenye bio yake kuna link ama you tube...ngoma inaitwa MZURI PESA...nasema hiviii ni hayo tu kwa leo..ahsanteni".Ameandika FA.