Thursday, September 22, 2016

PICHA:Mwenye hereni iliyokutwa chumbani kwa Diamond abainika.

 Mama watoto wa Mwanamuziki Diamond Platnumz,Zari The Boss Lady ameendele kutupa madongo kwa wanawake anaohisi wanatoka kimapenzi na Diamond baada ya kupost video kupitia mtandao wa "Snapchart" akiandika ujumbe kwenda kwa mwanamke anaedai ameacha hereni kwenye moja ya vyumba vyake bila kumtaja jina.

 Kupitia mitandao ya kijamii kumwekua na picha inayosambaa ikionesha picha ya hereni inayodaiwa kukutwa kwenye moja ya vyumba vya nyumba ya Diamond,Madale Tegeta huku upande wa pili ikionekana sura ya Mwanamitindo Hamisa Mabeto ambae hereni aliyovaa katika picha hiyo inafanana na hereni iliyozua kasheshe.






  Posts hizo za Zari zinaendelea kukuza tetesi za muda mrefu juu ya  usaliti kwenye  mahusiano yake w na Diamond hivyo pengine Mwanamama huyu ambae ana ujauzito wa pili kwa Hit maker wa singo ya "Kidogo",ameamua kuchukulia poa kuivumilia tabia ya Diamond japo suala hili linaweza kuchafua hali hewa kwenye mahusiano ya mastaa hawa.
Ikumbukwe kuwa kwa muda sasa Mwanamitindo Hamisa Mabeto amekua akiandamwa na skendo ya ku-share kitanda na Diamond ambae amekua akikanusha madai hayo,ambapo hata hivyo Mwanamuziki huyo amekuza tetesi hizo mara baada ya Hamisa kuonekena kama "Video Queen" kwenye video ya wimbo mpya wa Diamond aliomshirikisha Ray Vany unaofahamika kama "Salome"




Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.