Gari mpya imeingia sokoni kwa dola za
Kimarekani 15,000, na imekuja na muonekano tofauti kabisa na gari
nyingine unazozifahamu. Yenyewe inatumia umeme na inatumia matairi
matatu kama bajaji lakini inatumika na mtu mmoja pekee.
Gari hii imetengenezwa na Kampuni kutoka
Canada, inayofahamika kama kama Electra Meccanica. ambapo itaanza kuwa
barabarani ifikapo mwaka 2017.Gari hili limepewa jina SOLO kutokana na kuwa na uwezo wa kubeba mtu mmoja tu.
Imetengenezwa sio kwa lengo la
kukuhamisha wewe kutoka katika kutumia gari nyingine,bali
kukurahisishia mizunguko yako ya hapa na pale.
Inauwezo wa kutembea kwa spidi ya maili
80 kwa saa,Ikiwa na betri ya yenye madini aina ya lithiam
inayojichaji kila baada ya umbali wa maili 100. 100.Muda unaotumia kuchaji gari hiyo unategemea na uwezo wa chaji
yako ( voltage). 220V utakaa mpaka masaa 3 kuicharge, na kwa 110V itakaa
mpaka masaa sita ikiwa kwenye chaji.
Tazama picha tofauti za gari hilo ;