Mwanamitindo na mhanga wa shambulizi la tindikali raia wa India,Rashma Quereshi ameushangaza ulimwengu kwani licha ya shambulizi la tindikali alilopata na kupoteza jicho lake,bado hakukata tamaa ya kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanamitindo.Kwa kuthibitisha hilo,Mwanamitindo huyo Sept.9 mwaka huu alitokea kwenye onesho la mavazi linalofahamika kama FTL Moda Show lilifanyika Jijini New York nchini Marekani.
Reshma anadai kuwa alipoteza jicho lake miaka miwili iliyopita baada ya kumwagiwa tindikali na kaka yake akishirikiana na marafiki zake wawili wa kiume bila kuelezea lengo la ndugu yake huyo kumfanyia unyama huo na kuongeza kuwa licha ulemavu alionao amemua kuendelea na mipango yake ya kimaisha aliyojiwekea ili kuwahamasisha wahanga wengine wa kumwagiwa tindikali kujitokeza hadharani na kujisikia sehemu ya jamii.
Picha kwa hisani ya : Reuters