Kundi moja la wabunge nchini Uingereza limetoa wito wa kuhalalishwa kwa matumizi ya bangi kwa sababu za kimatibabu nchini humo.
Kundi hilo linalojumuisha wabunge kutoka
vyama mbalimbali vya kisiasa, na ambalo limekuwa likitetea mageuzi
kuhusu matumizi ya dawa, limesema kuna ushahidi wa wazi kwamba matumizi
ya bangi ya manufaa katika kutibu baadhi ya matatizo ya kiafya, yakiwemo
maumivu makali na pia kuondoa wasiwasi.
Wabunge hao wanasema tayari maelfu ya
watu huvunja sheria kwa sasa na kutumia bangi kama dawa. Na kwasababu
inasaidia hawaoni tabu kufanya matumizi hayo ya bangi kuwa halali. Na
iwaruhusu madaktari kutoa ushauri wa kutumia bangi endapo mgonjwa
atakuwa na uhitaji.
Aidha, Wizara ya Mambo ya Ndani nchini humo imesema kufikia sasa hakuna mipango ya kuhalalisha matumizi ya “dawa hiyo hatari”.
Taasisi ya Taifa ya Afya nchini
Uingereza imetahadharisha wananchi kwamba bangi ina madhara makubwa kwa
mwili, ikiwemo uwezo wa mtu kuendesha gari kupungua na vile vile
inaathiri mapafu na afya ya akili, huathiri uwezo wa mtu kuzaa na mbaya
zaidi bangi huathiri watoto ambao bado hawajazaliwa.
Asilimia (9%) ya watu wanaotumia bangi mpaka sasa
ni watu tegemezi, japo ndiyo si asilimia kubwa kulinganishwa na watu
wanaotumia tumbaku (32%) na wale wanaotumia pombe kama kilevi (15%). Na
kutahadharisha idadi hiyo huenda ikaongezeka endapo bangi itahalalishwa.
Licha ya yote hayo, wabunge hao wanasema
wametathmini na kupata ushahidi kutoka kwa wagonjwa 623. Na vile vile
waliweza kuzungumza na wataalamu kutoka nchi nyingi duniani na
wamegundua bangi inaweza kufaa sana kama dawa. Matumizi ya bangi kwa
sababu za kimatibabu yamehalalishwa katika majimbo 24 nchini Marekani na
pia nchi kama Canada na Israel wao pia wameshahalalisha. Huku nchi
zaidi ya 10 duniani kwa sasa wamesharuhusu matumizi ya bangi kwa sababu
za kiafya.
Chanzo– BBC